Monday, 9 December 2013

MSHINDI WA TUSKER PROJECT FAME



Mshiriki Hope toka Burundi amejikuta akianguka chini kwa mshituko wa furaha ulimkuta baada ya kuibuka kidedea kwa kutangazwa mshindi wa Tusker Project Fame na kujinyakulia kitita cha Shilingi 5,000,000/= za Kenya.


Mashindano hayo yaliyomalizika Jana yamemwacha Hope katika taharuki huku akiwabwaga wenziye; Hisia (Tanzania), Patrick (Rwanda),Wambura (Kenya), Daisy (Uganda),Amos & Josh wa Kenya.

Sauti ya pekee ya kijana huyo imeibua thamani yake katika tasnia ya muziki,Hope hakuwahi kufanya video shooting ya wimbo wowote zaidi ya ule uliompatia ushindi wa Tusker.

No comments:

Post a Comment