UDAKU


Nora adai Ray anamfitini kwa sababu alimkataa, asema alimharibia kwa Kanumba. Msikilize hapa




Muigizaji wa kike aliyefanya vizuri kupitia kundi la Kaole Sanaa Group, Nuru Nassoro aka Nora amedai kuwa amekuwa akifanyiwa fitina na muigizaji mwenzake Vicent Kigosi aka Ray kwa kuwa aliwahi kumtaka kimapenzi akamkataa.

Nora amefunguka kupitia kipindi cha Filamonata cha 100.5 Times Fm na kudai kuwa Ray amekuwa akimbania hata kwenye baadhi ya makampuni ambayo anapeleka kazi zake.

“Mpaka kwenye kampuni ambayo nimepeleka kazi nimeshawahi kusikia wanasema, wakaniahidi sana mpaka nikawakubalia walichokuwa wanataka wao. Lakini yeye (Ray) alitanguliza movies zake, akasema ana movie zake sijui kitu gani..” amelalamika Nora.

Ameeleza kuwa Ray amewahi kumbania kufanya kazi na marehemu Kanumba, na hata Mtitu sababu ikiwa ile ile kumkataa kimapenzi.

“Alishawahi..kitu ambacho kwangu kimeshawahi, sasa mimi sijui yeye ni alivyo au kwangu..ila mimi alinibania kwa sababu nilikuwa simtaki, akaniharibia kwa Mtitu. Kanumba kipindi kile alikuwa anamsikiliza sana Ray, akamwambia asifanye kazi na mimi. Hata Kanumba alikuwa ameelewana na mimi Ray akamwambia ‘achana naye’.” Nora ameiambia Filamonata.

Amedai kuwa wanaume wengi katika tasnia ya filamu wanamekuwa wanawanyanyasa wanawake kwa kuwata kimapenzi, na kwamba inakuwa ni mambo ya ndani ambayo sio rahisi kufahamika.

“Ikitokea hivyo inakuwa ni mambo ya ndani sana kiasi kwamba hata mwenzako anakwambia kwamba utaona kama utaendelea kuwa flani.” Nora amefunguka.

Nora amedai kuwa ana kazi nyingi lakini ameshindwa kuziingiza sokoni kwa sababu ya kubaniwa.

Hata hivyo Nuru Nassoro aka Nora amesema ameshasamehe na anaendelea na kazi zake.





                                 BIFU LA PREZOO NA HUDDAH LAFIKIA PABAYA





Bifu lao limefikia pabaya mpaka kujibizana kwenye mitandao ya twitter  na chanzo ni mrembo huyo kumka kila kitu japo umri umeeashifu king wa mabling bling kuwa hana hela na pia anamtegemea mama yake kwa kila kitu japo umri umeenda sana

              CHEKI HAPA




Ray C: Wakati naumwa sikuwahi kupigiwa simu na msanii mwenzangu







Rehema Chalamila aka Ray C jana alifunguka kupitia kipindi cha Mkasi jinsi ambavyo wasanii wenzake walimtenga wakati alipokuwa amelazwa hospitali kupatiwa matibabu ya ‘uraibu’ (addiction) wa madawa ya kulevya.

Ray C alisema japokuwa mama yake alitoa kwa umma mawasiliano yake na maelekezo ya namna ya kumsaidia, simu hiyo iliyokuwa busy saa 24, ilikuwa ikipokea simu na ujumbe kutoka kwa mashabiki wake pekee na sio msanii yeyote anayemfahamu.

Muimbaji huyo aliyewahi kutamba na vibao vingi vikali vikiwemo ‘Niwe Nawe Milele’ Uko Wapi na Sogea Sogea, alisema hiyo ilimpa funzo kuwa mtu maarufu huwa na marafiki pale tu anapokuwa juu lakini akipata matatizo hutengwa na hata watu wake wa karibu.

Katika kipindi hicho pia, Ray C aligusia jinsi ambavyo Lord Eyez alimuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ambapo alikuwa akimchanganyia unga kwenye bangi bila ya yeye kufahamu na kwamba alifanya hivyo kwa mwaka mzima.

Alisema baada ya kujigundua kuwa tayari ameingia kwenye tatizo kubwa aliamua kuchukua uamuzi wa haraka wa kuachana na rapper huyo ingawa anasema alikuwa akimpenda kwa dhati.

Katika hatua nyingine, Ray C alisema hakuna mtu anayeweza kumshukuru zaidi kama Rais Jakaya Kikwete ambaye alimuelezea kuwa ni mtu mwenye moyo wa kipekee kwakuwa amemsaidia kwa hali na mali na kumtoa kutoka kwenye janga la uteja.

Aliongeza kuwa Rais Kikwete amekuwa akiwasaidia vijana wengi wenye matatizo hayo na sio yeye peke yake.

Alisema kwa sasa tayari amesharekodi nyimbo takriban 12 na watayarishaji tofauti wa muziki akiwemo Tudd Thomas na Ema The Boy na kwamba hivi karibuni ataachia wimbo wake mpya.

No comments:

Post a Comment