KOCHA wa Manchester United, David Moyes amesema hakuna ukweli wowote kwamba straika Robin van Persie hafurahii tena kuendelea kukaa Old Trafford baada ya kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Newcastle United juzi Jumamosi.
Mabingwa hao watetezi wamepoteza mechi tano kwenye Ligi Kuu England hadi sasa, idadi ambayo walipoteza kwa msimu mzima uliopita.
Van Persie alirejea kwenye kikosi cha kwanza katika mechi hiyo baada ya kuwa nje ya uwanja kutokana na kuwa majeruhi.
Kumekuwa na madai kwamba staa huyo ameandika barua ya maombi ya kutaka ahame timu hiyo kwenye usajili wa Januari mwakani.
“Hizi habari hazina ukweli wowote. Sijui niseme kitu gani chenye mkazo zaidi, lakini ukweli hakuna kitu kama hicho,” alisema.
Moyes alisema tatizo linaloendelea Manchester
United halisababishwi na yeye kwamba anataka kuibadili timu hiyo sana
baada ya kuchukua mikoba ya Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu
uliopita.
Moyes alifanya usajili mmoja tu wa kumsajili Marouane Fellaini kutoka Everton kwa uhamisho wa Pauni 27.5 milioni.
united ni shidaaaa
ReplyDeletebt am united ever GGM