Ile collabo iliyofanya vizuri mwaka 2012 kati ya Shetta na Diamond Platinumz inajirudia tena mwishoni mwa mwaka huu,ambapo wasanii hao wawili wameamua kuingia studio na kutengeneza wimbo mpya unaoitwa kwa jina la Mama Qayllah.
Shettta ameiambia tovuti ya Dj fetty kuwa tayari ameshafanya ngoma hiyo mpya na Diamond Platinumz inayoitwa Mama Qayllah ambayo imetayarishwa na Shedy Clever wa Burn Records.
'Napenda kutoka shukrani za dhati kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva kwa kunielewa kwa kile ninachokifanya katika tasnia ya muziki pia ningependa kuwaambia kwamba ninatarajia kuachia wimbo mpya hivi karibuni ambao nimefanya na Diamond,ngoma inaitwa 'Mama Qayllah' producer aliyesimamia Vocal,Mixing ni Sheddy Clever wa Burn Records,kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula, hapa Shetta ama Baba Qayllah pale Diamond wa Wasafi Classic Baby,aahaha hatari'Alisema Shetta.
Kaa Tayari kwa ujio huo mpya kutoka kwa Shetta ft Diamond 'Mama Qayllah'
No comments:
Post a Comment