Tuesday, 19 August 2014

TOKA LIBERIA : WEZI WAIBA MAGODORO NA MASHUKA KATIKA HOSPITALI YA WAGONJWA WA EBORA ,







Polisi nchini Liberia wanaendelea kuwasaka wagonjwa 17 waliotoroka baada ya kliniki maalum ya wagonjwa wa Ebola kuvamiwa na kuporwa Jumamosi iliyopita.

Waziri wa habari wa Liberia, Lewis Brown amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa wavamizi hao waliondoka na ugonjwa wa Ebola na kuusambaza kwa kuwa walibeba mashuka na magodoro yaliyokuwa yakilaliwa na wagonjwa hao huku yakiwa na majimaji ambayo huusambaza.
Kutokana na tukio hilo, serikali ya nchi hiyo imeagiza eneo hilo kuwekewa vizuizi ili kuepuka kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo katika maeneo mengine.
Wakazi wa eneo hilo wameeleza kuwa wavamizi hao walipokuwa wanatekeleza tukio hilo walisikika wakidai kuwa hakuna ugonjwa wa ebola na kwamba hizo ni hadithi za kusadikika za imani.

No comments:

Post a Comment