He is a Ordinary Diploma Of Computer Science also holder of BSc(Cs)Bachelor of Science in Computer Science from ST. .JOSEPH UNIVERSITY to RUCU. The C.E.O and founder of I.T MAN SOLUTION Tz1 with enough knowledge in Computer mainteance and softwares, android tricks, web designing and graphics design, part-time blogger and softwares distributor with enough knowledge on entrepreneurship. Reach him 24/7 through WhatsApp 0716 68 43 67 and 0762324735 itmansolution2016@gmail.com.
Tuesday, 19 August 2014
#Mrembo Amwagiwa Mafuta ya Moto Usoni kisa mume wa mtu
Mwanadada aliyefahamika kwa jina moja la Mbuva, mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar, hivi karibuni amejikuta akiharibiwa uso wake kwa kumwagiwa mafuta ya moto na shosti wake aitwaye Mama Sofia, kisa kikidaiwa ni mume wa mtu.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo inadaiwa mama Sofia alimfanyia mwenzake unyama huo akimtuhumu kutembea na bwana wake.Akisimulia ilivyokuwa, Mbuva alisema:
“Mama Sofia alipewa maneno ya uongo kwamba akiwa safarini eti nilitembea na bwana yake.
“Siku ya tukio alinipigia simu akaniita kwake, nilikuwa sipajui ila akanielekeza, ile nafika tu majirani zake wakamwambia mimi ndiye nilikuwa nakwenda kulala pale na mume wake.
“Nikajaribu kujitetea lakini hakunielewa. Nikaondoka, baadaye akaniita tena, kufika pale nikakuta ugomvi kati ya mama Sofia na mumewe, ghafla mama Sofia akatoka akiwa na kikombe cha mafuta ya moto akanimwagia usoni.
“Nikaanza kupiga kelele, watu wakajaa ndipo tukachukuliwa wote na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mazizini na tukaandikisha, mimi nikakimbizwa hospitali. Ameniharibu uso wangu bila kosa, Mungu atanilipia kwani naamini malipo ni hapahapa duniani.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment