He is a Ordinary Diploma Of Computer Science also holder of BSc(Cs)Bachelor of Science in Computer Science from ST. .JOSEPH UNIVERSITY to RUCU. The C.E.O and founder of I.T MAN SOLUTION Tz1 with enough knowledge in Computer mainteance and softwares, android tricks, web designing and graphics design, part-time blogger and softwares distributor with enough knowledge on entrepreneurship. Reach him 24/7 through WhatsApp 0716 68 43 67 and 0762324735 itmansolution2016@gmail.com.
Saturday, 30 August 2014
#DI MARIA KUANZA LEO DHIDI YA BURNLEY
Siku moja baada ya Angel Di Maria kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa klabu ya Manchester United ya England huku akikabidhiwa jezi yenye historia kubwa ndani ya klabu hiyo (namba 7), mwanasoka bora wa ulaya na mchezaji wa zamani wa United, Cristiano Ronaldo amezungumza juu ya Di Maria kwenda Old Trafford pamoja na kupewa jezi namba 7.
Ronaldo ambaye aliondoka Man United mnamo mwaka 2009 kwa ada ya uhamisho ambayo iliweka rekodi ya £80m amesema hana wasiwasi wa Di Maria kufanikiwa ndani ya United.
“Uhamisho huu ni kitu kizuri kwake.” Ronaldo aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Monaco.
“Manchester [United] ni moja ya klabu kubwa duniani, ni sehemu nzuri kwa Di Maria na namtakia kheri na mafanikio, Di Maria ni mchezaji mzuri sana, anastahili kuichezea United.”
Alipoulizwa juu ya Di Maria kupewa jezi namba 7 aliyokuwa akivaa alipokuwa Man United, Ronaldo alisema: “Nilimwambia, ‘jezi No.7 ina maana kubwa ndani ya United, lakini nadhani ataweza kubeba uzito wa jezi kwa sababu ni mchezaji mzuri sana.”
Di Maria anaweza kuanza kuichezea Man U kesho kwenye mchezo dhidi ya Burnley.b
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment