Monday, 28 July 2014

HII NDIYO NDEGE ILIPATA HITILAFU MDA SI MREFU NCHINI MAREKANI




Mpaka sasa kuna habari nne kubwa za ndege ambazo zimetokea ndani ya kipindi cha siku 9 zilizopita, kuna ajali ya ndege tatu ambazo ni ile ya Malaysia, Mali na Taiwan ambapo kwenye kisa kilichofata ni cha ndege moja kulazimika kurudi ilikorukia baada ya kijana raia wa Canada kusema ana mpango wa kuilipua nchi yake kwa sababu anaichukia.

Sasa tukio jingine la saa kadhaa zilizopita ni kuhusu ndege ndogo ya abiria ambayo imelazimika kutua kwa dharura ufukweni huko Venice Florida Marekani baada ya kupata tatizo ikiwa angani na rubani kuona hakukuwa na uwezekano wa kufika uwanja wa ndege alikofanya mawasiliano.


Kutua huku kwa dharura kumesababisha kifo cha Mwanaume mmoja alikua akitembea ufukweni huku mtoto wake wa kike akijeruhiwa vibaya kwenye hii ajali.

No comments:

Post a Comment