Monday, 28 July 2014

#FAHAMU RONALDO ALICHOMJIBU LIL WAYNE KUHUSU KU MMANAGE




Baada ya Jay Z kufungua kampuni ya kusimamia Wanamichezo na kuanza kupata mafanikio kupitia biashara hiyo, mkali mwingine wa hip hop Lil Wayne ameripotiwa kufungua kampuni ya usimamizi wa Wanamichezo ambapo Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ametajwa kuwa mchezaji wa kwanza kusainiwa na kampuni hiyo.

Taarifa zilizotoka zilisema Lil Wayne kupitia kampuni yake atakuwa akishughulikia masuala yote ya kibiashara ya Ronaldo ndani ya Marekani kwa mujibu wa TMZ.

Kampuni hiyo ya Weezy inatajwa kuwa ingefanya kazi na kampuni ya PolarisSports, kampuni dada na CAA na GestiFute, taasisi ambayo wakala wa Ronaldo – Jorge Mendes ndio anaiendesha lakini pamoja na headlines zote hizo, Ronaldo amekanusha taarifa hizo na kusisitiza kwamba timu yake ni ileile na itakua hiyohiyo.


Ronaldo yupo chini ya kampuni ya usimamizi wa wachezaji ya GestiFute ambayo pia inamwakilisha Jose Mourinho, Pepe, James Rodriguez, Moutinho, Falcao, Nani na wachezaji wengine wengi wa Ureno na Amerika ya kusini.

No comments:

Post a Comment