Tuesday, 4 March 2014

Sikiliza wimbo mpya wa Jux 'Nitasubiri', unaweza kudhani amemuimbia Jackie Cliff



Mkali wa RnB, Jux ameachia wimbo mpya unaoitwa ‘Nitasubiri’ ambao ni dhahiri kwamba utakuwa wimbo mzuri kwa mashabiki wake kama ilivyokuwa kwa Uzuri wako.

Lakini kwa kuzingatia tukio la kutokuwa karibu na mpenzi wake Jackie Cliff, ukisikiliza mashairi ya wimbo huu unaweza kudhani labda Jux amemuimbia moja kwa moja mrembo wake.

“Ushanifanya niwe Mental…mental hata chakula sikitamani. I wish ungekuwepo Apple, tuchezecheze wangu mwandani.” Anasikika Jux kwenye kibwagizo cha wimbo huo.

“Mi nakosa Amani namuomba Mola wewe urudi nyumbani, ufananishwe na nani nimemiss ulivyonipa zamani. Subira mola amenipa, mimi kwa penzi lako...”

Hata hivyo, Jux aliuambia mtandao wa kuwa wimbo huo hakumuimbia Jackie Cliff kama wengi walivyoanza kufikiria baada ya kuona jina la wimbo.

“Nitasubiri ni wimbo ambao ni kweli ni nyimbo ya mapenzi. Inaelezea kwamba kusubiri kwa mapenzi kuna aina nyingi ujue, kuna safari, kuna wewe kuondoka kumuacha mpenzi wako, mimi nimejaribu kufanya utofauti tu kwa sababu nimeimba nyimbo nyingi sana.” Alisema Jux.

No comments:

Post a Comment