He is a Ordinary Diploma Of Computer Science also holder of BSc(Cs)Bachelor of Science in Computer Science from ST. .JOSEPH UNIVERSITY to RUCU. The C.E.O and founder of I.T MAN SOLUTION Tz1 with enough knowledge in Computer mainteance and softwares, android tricks, web designing and graphics design, part-time blogger and softwares distributor with enough knowledge on entrepreneurship. Reach him 24/7 through WhatsApp 0716 68 43 67 and 0762324735 itmansolution2016@gmail.com.
Tuesday, 4 March 2014
KUFURU: Wayne Rooney agawa saa ya Sh40 milioni Dubai
MANCHESTER,ENGLAND
YUPO wapi yule aliyesema pesa ni sabuni ya roho? Hakukosea sana. Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney, ameonyesha kufuru kubwa ya pesa muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa Pauni 300,000 kwa wiki.
Akiwa Dubai na wachezaji wenzake katika mapumziko ya kipindi cha joto hivi karibuni, inadaiwa kuwa Rooney alitoa saa yenye thamani ya Pauni 20,000 ili ishindaniwe katika shindano la kirafiki la mchezo wa gofu miongoni mwa wachezaji wenzake na wafanyakazi wa timu hiyo.
Rooney ambaye ni shabiki mkubwa wa gofu, alijaribu kunogesha shindano hilo ndani ya kambi ya United kwa kutoa saa hiyo kwa mtu yeyote ambaye angeshinda hata kama ni mfua jezi wa klabu hiyo.
Bahati ya Mtende ilimwendea kocha wa makipa wa Manchester United, Chris Woods, ambaye alihamia timu hiyo katika kipindi cha majira ya joto akitokea Everton ambako alikuwa pamoja na kocha wa sasa wa United, David Moyes.
Kitendo hicho kiliwashangaza maofisa wa United pamoja na wachezaji wa timu hiyo katika kambi yao ya Dubai ambayo iliwekwa kwa ajili ya kuwapumzisha wachezaji ambao msimu huu wanaonekana kuchemsha.
Huu ni mwendelezo wa matanuzi kutoka kwa wachezaji wenye mishahara mikubwa barani Ulaya ambao wamekuwa hawahofii kununua chochote wanachojisikia.
Nyota wa kimataifa wa Cameroon anayekipiga Chelsea, Samuel Eto’o, naye ni mmoja kati ya wachezaji waliowahi kufanya matanuzi ya aina hii kwani mwaka 2009 alijikuta akiwazawadia wachezaji wote wa timu ya taifa ya Cameroon saa aina ya Rolex, kila mmoja alipata.
Kila saa ilikuwa na thamani ya Pauni 29,000 na Eto’o alifanya hivyo mara baada ya Cameroon kufanikiwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Afrika Kusini. Ilikuwa ni furaha ya kuichapa Morocco mabao 2-0.
Kwa jumla, saa zote hizo ambazo zilinakishiwa kwa vito vya aina tofauti zilimgharimu Eto’o kiasi cha Dola 1.3 milioni ambazo alizilipa kupitia moja ya akaunti zake za kigeni barani Ulaya na kuwaacha midomo wazi wachezaji wenzake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment