Sunday, 2 February 2014

MOURINHO AANZA KUICHOKONOA MAN CITY KABLA YA MECHI YA KESHO





ose Mourinho ameendelea kuishambulia Manchester City huku wakiwa wanaenda kupambana Jumatatu katika uwanja wa Etihad Stadium.

Siku chache mara baada ya kudai kuwa Man City imekuwa na bahati kutokana na maamuzi mabovu ya marefa msimu huu,meneja huyo wa Chelsea amesisitiza kuwa vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza bado wapo chini ya mafanikio ukilinganisha na jinsi walivyowekeza.

Man city walishinda ubingwa wa EPL mwaka 2012 katika kipindi cha miaka 44,lakini wameweza kufika hatua ya 16 bora katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya wakitaraji kukutana na Barcelona.

Mourinho alisema kuwa wameshinda taji la ligi kuu ya Uingereza,pamoja na vikombe kadhaa ila Ulaya wameshindwa kufanya vizuri kabisa.

Huku akisisitiza kuwa walifanya vibaya sana kwa misimu iliyopita katika ligi ya mabingwa na hata Europa ligi.

Lakini akasisitiza kuwa timu yao ni nzuri,kikosi chao ni bora na kwa kawaida ilibidi washinde vikombe vingi zaidi.

Pia Mreno huyo alimtania Manuel Pellegrini kwa kusema kuwa kitu cha kwanza kuzingatia ili ufanikiwe Ulaya ni kujua sheria za michuano unayoshiriki akiongelea jinsi Man City walivyoshindwa kupiga mahesabu ya kupata goli moja zaidi katika mchezo wa mwisho dhidi ya Bayern Munich ili kuweza kuongoza kundi na kuikwepa Barcelona katika 16 bora.



Mourinho aliongeza kuwa Man City wananafasi nzuri katika mbio za ubingwa msimu huu ingawa akadai yeye anafurahia maisha yake Chelsea kwasasa kwani anatengeneza timu ya baadae na ya muda mrefu zaidi.

Na kusisitiza kuwa anafikiri msimu ujao ndiyo utakuwa mzuri sana kwake na kwa Chelsea,kwani anachoangalia ni kujenga timu ya kudumu na siyo kusubiri msimu uishe halafu anunue wachezaji wapya na kuuza wengine na kuanza na timu mpya kabisa.

No comments:

Post a Comment