He is a Ordinary Diploma Of Computer Science also holder of BSc(Cs)Bachelor of Science in Computer Science from ST. .JOSEPH UNIVERSITY to RUCU. The C.E.O and founder of I.T MAN SOLUTION Tz1 with enough knowledge in Computer mainteance and softwares, android tricks, web designing and graphics design, part-time blogger and softwares distributor with enough knowledge on entrepreneurship. Reach him 24/7 through WhatsApp 0716 68 43 67 and 0762324735 itmansolution2016@gmail.com.
Wednesday, 19 February 2014
Kilichozungumzwa na Nape Nnauye kuhusu adhabu waliyopatiwa wakina Lowasa.
Kuna taarifa kuhusiana na baadhi ya Wabunge wa Ccm ambao wamesemekana kuwa kwenye adhabu ambayo mfano wake ni kama kifungo cha nje kwenye Chama Cha Mapinduzi.
Wabunge hao wanaosemekana ni wale walioonekana kuanza kutoa nia yao ya kugombea urais hadharani kuwa ni pamoja na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa,Waziri Mkuu wa zamani Fredrick Sumaye na Mbunge wa Sengerema William Ngeleja.
Kupitia kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm Katibu wa Itifaki na Uenezi wa Ccm Nape Nnauye amesema kuwa wabunge hao kwa sasa ‘Tafsiri yake ni rahisi tunazo kanuni za usalama na maadili ya chama za mwaka 2010,ni za siku nyingi ila zimekua zikirekebishwa kila baada ya muda fulani ili kukidhi mahitaji ya wakati’
‘Kanuni hizo zinatafsiri adhabu waliyopewa maana yake mtu anaepewa adhabu hiyo atakua chini ya uangalizi wa chama kwa kipindi cha miezi 12 na inasema hivi Mwanachama aliyepewa adhabu ya onyo kali atakua katika hali ya kuchunguzwa kwa muda usiopungua miezi 12 ili kumsaidia katika jitihada zake za kujirekebisha’
‘Sasa katika kipindi cha uchunguzi yapo mambo mtu hatotakiwi kufanya,kwa mfano ukiwa chini ya uchunguzi hutoruhusiwa kugombea chochote katika kipindi hicho cha uchunguzi utatakiwa kusubiri hadi hiko kipindi kiishe,tafsri ni kama kifungo cha nje ambacho unakuwa umebanwa pengine hutakiwi kusafiri’
‘La pili ni kutofanya kosa la kimaadili kwa kipindi hicho endapo ukifanya adhabu inaongezeka na ukimaliza kifungo kikaisha wanakwenda kwenye kikao wanasema huyu mtu amejirekebisha sasa hivi yuko huru au huyu mtu hajajirekebisha tuendelee kumuangalia’.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment