Wednesday, 8 January 2014

UVUTAJI WA SIGARA WAWAVUTIA WENGI





Idadi ya wavutaji wa sigara duniani imeongezeka kwa karibu bilioni moja kwa mujibu wa takwimu mpya.

Watafiti walioandika katika jarida la Shirika la madaktari la Marekani wanasema hata hivyo kuwa idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na ongezeko la watu kwa ujumla duniani na kuelezea haja ya juhudi zaidi kufanyika kuwazuia watu kuwa na tabia hiyo.

Idadi ya watu wanaovuta sigara kila siku duniani imepanda kwa kiwango cha watu takriban milioni 250 million kati ya mwaka 1980 na 2012, kwa mujibu wa ripoti .

Katika nchi kama vile Urusi ,Indonesia na Timor ya Mashariki , zaidi ya nusu ya wanaume wana tabia ya kuvuta sigara kila siku.

Baadhi ya maeneo yenye idadi ndogo ya wavutaji wa sigara ni katika visiwa vya Caribbean vya Antigua na Barbuda ambapo mtu mmoja kati ya 20 huvuta sigara kila siku.

Watafiti wanasema kuongezeka kwa kiwango cha wavutaji wa sigara kinatokana na ongezeko la watu duniani.

Lakini licha ya kuongezeka kwa kiwango cha uvutaji sigara , kiwango cha watu wanaovuta sigara duniani kimepungua. Idadi ya Wanaume wanaovuta sigara imepungua kwa asilimia 10 tangu mwaka 1980, na wanawake wamepunguza uraibu huo kwa asilimia 4.

Shirika la afya duniani linasema vifo vya mamilioni ya watu vinaweza kuepupika kwa nchi zaidi kuweka hatua kama vile kuongeza kodi ya sigara, kupiga marufuku uvutaji sigara katika maeneo ya umma na kuweka onyo kwenye paketi za sigara

No comments:

Post a Comment