
Aliyekuwa msanii wa kundi la G-Unit rapper Mazaradi Fox amepigwa risasi ijumaa ya tarehe 3 January 2014 akiwa maeneo ya nyumbani kwao Queens, New York. Fox amefariki akiwa na miaka 42.
50 Cent ametoa pole kwa familia ya Fox na kusema Maombi na mawazo yake yako nao.
Fox amepigwa risasi mida ya ijumaa saa kumi usiku, mtu asiye julikana alipita na gari Aina ya SUV na kumimina risasi kwenye eneo alilokuwa Fox.
Rapper huyu alitia wino mkataba na G unit mwaka 2007, ila hakuwahi kutoa album ndani ya Lebel hio na mwaka 2008 alijitoa G Unit.
No comments:
Post a Comment