Friday, 10 January 2014

Msanii Diamond Platinum Akiri Kuikose Magic Fm, Aomba Radhi Live Kupitia Kipindi Cha DalaDala Beats


Msanii Diamond Platinum Akiri Kuikose Magic Fm, Aomba Radhi Live Kupitia Kipindi Cha DalaDala Beats




Msanii Mkali wa miondoko ya Kizazi kipya Bongo, Bongo Fleva Diamond Platinum Leo Amekiri kupitia Kipindi Cha DalaDala Beats Kupitia Radio Magic Fm Ya Dar Es Salaam Kuwa Alikuwa anatofauti na Radio Hiyo kutokana na mambo ya kibinadamu yaliojitokeza yaliosababisha kupishana kiasi kwa aliowaita wafanyakazi wenzie kutokana na kutegemeana katika Kazi yake

Msanii Huyo aliyetembelea Studio Za Magic fm Akiongozana Na mkubwa Fela Pamoja Na Babu Tale kwa nia ya Kuja kuomba Msamaha na kuweka mambo sawa alifunguka kupitia kipindi cha Daladala Beats Kinachoruka Magic Fm Kuanzia Saa saba mchana mpaka saa kumi jioni

Ni Takriban Mwaka Mmoja Na Nusu Tangu Nyimbo za Msanii Huyo Kuacha kuchezwa na kituo hicho baada ya Misunderstanding hiyo kujitokeza.

Tangu jana kupitia vipindi mbaali mbali nyimbo za Diamond Zimeanza Kuskika Tena kupitia kituo hichi baada ya kurejesha tena maelewano baina ya kituo na msanii huyo

Diamond pia alizungumzia wimbo wake mpya wa My Number One Remix Aliofanya na msanii Davido wa Nchini Naijeri, na hilo ndo Pini jipya lililopo sokoni sasa kwa msanii huyo anayetajwa kuwa mkali zaidi bongo kwa sasa

Picha Wakati Msanii Diamond Akiwa Katika Studio Za Magic Fm Kuyamaliza

source - salmamsangi

No comments:

Post a Comment