Friday, 10 January 2014

Mchawi aanguka huko Kahama

Kikongwe mwenye umri kati ya miaka 85 hadi 90 ambaye bado hajafahamika jina lake amekutwa katika kijiji cha Nyashimbi kata ya Muhongolo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwa kile kinachodaiwa kuwa huenda ni mchawi aliyeanguka usiku wakati akiwa kwenye safari zake angani.

Kikongwe huyo baada ya kufikishwa kituo cha polisi
Kwa mujibu wa wakaazi wa Kijiji hicho bibi huyo ameonekana leo majira ya saa 12 asubuhi akiwa katika vichaka vilivyo kando ya barabara na alipoulizwa aliongea kidogo tu kuwa anatoka Kijiji cha Nyihogo wilayani Kahama.

Kikongwe huyo akiwa chini huku amezingirwa na kundi la wananchi

Akiwa amelala chini kwa kile kinachodaiwa ni njaa

No comments:

Post a Comment