Msururu wa matokeo maaya ya klabu ya Manchester United leo umekomeshwa na mchezaji Adnan Januzaj aliyewapa wachezaji wenzake matumani baada ya kushinda Swansea mabao mawili kwa nunge.
Adnan mwenye umri wa miaka 18 hakucheza katika mechi ya wikendi iliyopita, katika raundi ya tatu ya kombe la FA Man U waliposhindwa.
Aliweka wazi thamani yake kwa klabu hiyo aliposaidia vijana wa Moyes kuingiza mabao mawili kwa pasi zake murwa kwa Antonio Valencia na Danny Welbeck.
Bila shaka mchango wake umerejesha vijana wa Moyes katika mkondo wa ushindi, baada ya kipindi cha ukame wa mabao mara nne mfululizo.
Pia ushindi wa Jumamosi ulisaidia Man U kufunika aibu ya kushindwa mara nne nyumbani.
Danny Welbeck sasa ameingiza mabao sita katika mechi sita za Ligi ya Premier alizocheza.
Wakati goli la Antonio Valencia lilikuwa lake la kwanza nyumbani tangu mwaka 2011.
Man U sasa wako pointi nne nyuma ya Everton wanaoshikilia nafasi ya nne.
Bado wako pointi tisa nyuma ya Chelsea watakaocheza nao Jumapili ijayo na matumaini ni makubwa sasa kuwa huenda wakawa katika nafasi nzuri ya kunyakua kombe.
No comments:
Post a Comment