He is a Ordinary Diploma Of Computer Science also holder of BSc(Cs)Bachelor of Science in Computer Science from ST. .JOSEPH UNIVERSITY to RUCU. The C.E.O and founder of I.T MAN SOLUTION Tz1 with enough knowledge in Computer mainteance and softwares, android tricks, web designing and graphics design, part-time blogger and softwares distributor with enough knowledge on entrepreneurship. Reach him 24/7 through WhatsApp 0716 68 43 67 and 0762324735 itmansolution2016@gmail.com.
Monday, 13 January 2014
KIFO CHA UTATA..!! MSANII WA BONGO AUWAWA NCHINI CHINA, NI BAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AKIWA PAMOJA NA CANAL TOP..!!
MWANAMUIZIKI aliyepata kutamba na Bendi ya FM Academia ya jijini Dar es Salaam, Rapa, Haristot Shungu ameuawa nchini China huku kifo chake kikitawaliwa na utata mkubwa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichopo nchini China, rapa huyo alikamatwa uwanja wa ndege baada ya kugundulika kuwa amebeba madawa ya kulevya akiwa ameambatana na rapa mwingine wa Bendi ya Akudo Impact, Kanal Top na wote wawili kuhifadhiwa mahabusu.
“Tulijua kama Haristot alikamatwa pamoja na Kanal Top lakini ghafla juzi (Ijumaa) tukaambiwa kuwa amefariki dunia, hatujui kifo chake kimesababishwa na nini lakini mwili wake unaonekana kama vile aliungua na moto au mtu aliyechomwa sindano ya sumu,” kimesema chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo Amani liliwasiliana na Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Saadat na kumuuliza kama alikuwa na taarifa zaidi za Haristot.
Nyoshi alikiri kuwa marehemu alikuwa mwanamuziki wao na kudai kwamba kifo chake kimetawaliwa na utata mkubwa.
“Haristot alikuwa mwanamuziki wetu, mara ya mwisho aliaga kuwa anakwenda Ulaya kwa mchumba wake, nimeshangaa kusikia ameuawa nchini China kiukweli hakuna anayejua ukweli wa kifo chake,” alisema Nyoshi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment