WAZIRI AIKUMBUKA ZABURI YA 72
Dr. Mathayo David Mathayo
Waziri wa maendeleo ya mifugo na Uvuvi ambaye pia ni mtoto wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania David Msuya, Dr. Mathayo David Mathayo leo ameikumbuka Zaburi ya 72:2 ("Atawaamua watu wako kwa haki,Na watu wako walioonewa kwa hukumu").
Waziri David Mathayo amelikumbusha Bunge kwamba amejikuta akiusoma mstari huo na Zaburi hiyo ya 72 baada ya kuona kwamba ameonewa na wabunge na kuingizwa katika kashfa ya oparesheni tokomeza.
Hata hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametengua uteuzi wake pamoja na mawaziri wengine wa Wizara 3 ( Waziri Hamis Kagasheki(Waziri wa Maliasili na Utalii) , Emmanuel Nchimbi (Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi) na Shamsi Vuai Nahodha( Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa).
No comments:
Post a Comment