Thursday, 19 December 2013

JOKATEE AZINDUA "KIDOTI CLUB"


Mrembo, Muimbaji, Muigizaji wa filamu, Mtangazaji wa TV na Mjasiriamali nchini, Jokate Mwegelo aka Kidoti jana amefanya uzinduzi wa kile alichokiita ‘Kidoti Club’.


“Ni huduma za SMS, watu wanajiunga kwenye ‘Kidoti Club’ na watakuwa watapata tips mbalimbali za urembo, mitindo na mambo ya lifestyle, inspiration… na baadae kutakuwa na zawadi za kushindaniwa,”


Akiongelea maboresho aliyoyafanya kwenye nywele zake za brand ya Kidoti, Jokate amesema,
Tulipotoa bidhaa za mwanzo, honestly kuna watu walisema kuna vitu ambavyo walipenda viboreshwe zaidi na sasa hivi kweli vimeboreshwa. Packaging imeboreshwa, sasa hivi tumeweka kifungo.”

“Ni bidhaa ya nyumbani, ni bidhaa inayotengenezwa na mwanamke, kwa hiyo naelewa wanawake wanahitaji nini. Ni bidhaa ambayo bei yake sio kubwa lakini quality yake ni nzuri, mtu anaweza kuvaa kwa mwezi na isimuwashe kichwani. Kwa hiyo ni kitu ambacho tumekipackage vizuri, vilevile kina muonekano mzuri, rangi tumechagua nzuri. Kwa hiyo zinashindana vizuri tu na bidhaa za nchi nyingine,” ameongeza.

Jokate amesema bidhaa zake zimeshaanza kuvuka mpaka. “Nimelenga hasa East na Central Africa, kwa sababu nimeshaanza kupata order kutoka Burundi, Kenya..yeah kwa hiyo ni East na Central Africa. Kuhusu mikoani, sasa hivi mimi nadeal kwanza na Agents, agents wangu wengi wako Kariakoo na ndio wanaopeleka mikoani. Sijaanza kupeleka moja kwa moja mikoani, hiyo ndio njia ninayoitumia kupeleka mikoani.”

No comments:

Post a Comment