Monday, 16 December 2013

KAULI YA REGINALD MENGI KWA PROF MUHONGO








1. Nafurahi kwa nafasi ya kuwa nanyi leo kwa kuwa sekta binafsi itapata nafasi ya kipekee kesho tarehe 16 Desemba 2013, ya kuwa na mkutano chini ya Mhe. Rais Kikwete kama mwenyekiti.


2. Mimi binafsi nitapata heshima ya kushiriki kama kiongozi wa sekta binafsi chini ya TPSF. Lakini limekuwepo tatizo la mambo yaliosemwa na Mhe. Profesa Muhongo kunihusu ambayo ningependa niyafafanue ili nisiende kwenye kikao cha kesho zikiwepo fikra kwamba mambo hayo ni ya kweli.

3. Katika tarehe za mwanzo wa mwezi Septemba mwaka 2013 Mhe. Profesa Muhongo alinukuliwa akisema kwamba:



“Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu.”



4. Ukweli ni kwamba mimi siyo mbinafsi na pili sijawahi kuomba upendeleo wa kupewa kitalu cha gesi bali ninapigania Watanzania kwa ujumla.



5. Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu Lissu kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Mhe. Profesa Muhongo alitoa takwimu za kunihusu ambazo siyo sahihi.



6. Ukweli ni kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita mojaya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema.



7. Naomba nisisitize kwamba mimi binafsi nimeshapata nafasi kubwa ya kujiendeleza kibiashara. Ukweli ni kwamba ninachopigania leo ni juhudi ya kupanua wigo ili Watanzania wengi waweze kushiriki kama ilivyo kwenye Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004, (National Economic Empowerment Act, 2004) ambayo inatoa upendeleo maalumu kwa Watanzania katika rasilimali zao.



8. Ninamatumaini makubwa kwamba katika mkutano wa kesho ambao utatoa fursa kwa sekta binafsi kuzungumza na uongozi wa Taifa chini ya uwenyekiti wa Mhe. Rais utatuwezesha kupata muafaka wa ni jinsi gani tutashirikiana katika juhudi za kuwawezesha Watanzania kwenye nyanja mbalimbali za uchumi wetu.




Dkt. Reginald A. Mengi



Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment