Msanii wa hip hop nchini anaejulikana kwa jina la WAKAZI leo asubuhi majira ya saa 12 wakati anarudi zake nyumbani alinusurika kwa ajali mbaya ya gari kwa kugongwa na gari nyingine maeneo ya Victoria. Wakati mimi na Pancho tunarudi nyumbani tulikutana na ajali hiyo ikiwa ndio kama dakika 5 tu kutokea, dereva wa gari aliyesababisha ajali hiyo alikuwa amelewa sana mpaka akawa anashindwa kujielezea mwenyewe. Majira ya saa moja ndio waliweza kufika mapolice na kupia ajali hiyo na hatimae magari hayo kubebwa na kupelekwa Osterbay police. Kwenye ajali hiyo hakuna mtu yoyote aliyeumia.
Hii ndio gari ya Wakazi ikiwa imebebwa na sehemu iliyoumia ni upande ule mwingine sehemu yote na milangoni na tairi la nyuma lilipasuka.
No comments:
Post a Comment