Friday, 27 December 2013

CONFIRMED: ALIYEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA NI JACKIE CLIFF, MTANZANIA MWINGINE NA MNAIJERIA WALIKIMBIA



Rafiki wa karibu wa video vixen maarufu nchini, Jackie Cliff amethibitisha taarifa zinazoendelea kukua kwa sasa kuwa msichana aliyekamatwa na kilo 1.1 ya madawa ya kulevya aina ya Heroin huko Macau, China ni yeye.

Awali tuliandika kuwa pamoja na jina la mrembo huyo kutajwa na vyanzo vingi kuwa ni kweli amekamatwa, tulichelea kulitaja jina lake ili kuepusha kuandika habari isiyo na uhakika.

Rafiki huyo wa Jackie, ambaye pia ni rafiki mkubwa Jux mwenye uhusiano wa karibu na Jackie, Chief Rocka (kiongozi wa kundi la Rockaz) ameandika kupitia Instagram:

“I feel so sorry for jackie...God be with u and help u thru this one...we r human we make mistakes...wuldnt want to jump on judgin u like how other people do....this is Bad...2013 plz its enuf.”

Bong imoeongea kwa simu na Chief ambaye yupo masomo nchini China kujua undani wa tukio hilo.

“Amekamatwa kweli,” Chief ameiambia Bongo. “Nlivyosikia story ni kwamba ametoka Bongo akapita Thailand baada ya kutoka Thailand akaenda Macau, Macau ndio akamatwa. Mimi nilijua sababu nilipigia simu watu wa ubalozini baada ya kupata taarifa tu mara ya kwanza nikawapigia watu wa ubalozi nikawaambia ‘bana, ndugu yetu amekamatwa sasa nataka kujua process ikoje kama kuna kumuona au kama kuna chochote. Kuna ubalozi mwingine mdogo upo Hong Kong wao ndio wakaniambia mambo yalivyo kwamba alikuwa yupo yeye na watu wengine wawili Mtanzania na Mnaijeria, yeye ndo kakamatwa, hawa wengine baada ya kuona wanataka kukamatwa wakakimbia,” Chief ameeleza.

No comments:

Post a Comment