the QUARTZ Blog
Taarifa kutoka Jeshi la polisi kukamata watuhumiwa 13 wa Ujambazi
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam jana limetangaza kuanza oparesheni kubwa kwa ajili yakukabiliana na uhalifu katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka.
Oparesheni hiyo imeanza kufanikisha kukamata watuhumiwa 13 wa makosa ya ujambazi ambao kwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa wamekuwa wakijihusisha na utumiaji wa silaha na wameshafanya matukio ya uhalifu kwenye maeneo mbalimbali ndani na nje ya Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamishna wa polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova, amesema kuwa wahalifu wengi wamekuwa na mazoea ya kufanya uhalifu mwishoni mwa mwaka kuelekea sikukuu za krismas na mwaka mpya.
Alisema kuwa katika kipindi hiki hadi mwezi wa Desemba uharifu unaongezeka kutokana na watu kutafuta fedha, hali hiyo inapelekea uharifu kuongezeka na baadhi ya watu kupoteza mali zao.
Kutokana na hilo jeshi limefanikiwa kukamata kwa watuhumiwa wa ujambazi 13 ambao uchunguzi wa awali ulibaini kuwa wameshafanya mtukio kadhaa ya uhalifu maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
“Kipindi kama hiki kwa kawaida uharifu unapanda juu watu wanatafuta fedha, hakuna sababu ya kusubiri matukio makubwa ya uharifu yatokee ndipo tuanze kufanya kazi hiyo kama jeshi la polisi kazi yetu ni kulinda mali za raia” alisema Kova.
Aidha Kamishna Kova amewaasa wananchi na wafanya biashara kutosafirisha pesa kiholela na badala yake washirikiane na jeshi la polisi ili kuhakikisha ulinzi wa kutosha na kuepuka madhara yakiwemo vifo na majeruhi.
No comments:
Post a Comment