He is a Ordinary Diploma Of Computer Science also holder of BSc(Cs)Bachelor of Science in Computer Science from ST. .JOSEPH UNIVERSITY to RUCU. The C.E.O and founder of I.T MAN SOLUTION Tz1 with enough knowledge in Computer mainteance and softwares, android tricks, web designing and graphics design, part-time blogger and softwares distributor with enough knowledge on entrepreneurship. Reach him 24/7 through WhatsApp 0716 68 43 67 and 0762324735 itmansolution2016@gmail.com.
Sunday, 7 September 2014
MISTAKE : Scholes ,Beckhamu wadai Manchester United imechemsha kumuuza Welbeck
BAADA ya David Beckham, sasa ni zamu ya Paul Scholes. Nyota wote wawili hawa hawaelewi ni kwa nini Manchester United imeamua kumuuza Danny Welbeck kwenda Arsenal.
Welbeck aliyekulia United tangu akiwa na umri wa miaka sita alikamilisha uhamisho wa kwenda Arsenal siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Jumatatu usiku, huku akionekana kama mchezaji anayeweza kuziba pengo la Olivier Giroud aliyeumia.
Kuondoka kwa staa huyo wa England mwenye umri wa miaka 23 kumechukuliwa na wengi kama kupisha njia kwa staa wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka Monaco mchana wa siku hiyo.
Hata hivyo, licha ya ujio wa Falcao, Scholes anaamini kwamba bado Welbeck angeendelea kuwa mchezaji muhimu wa siku za usoni na kuondoka kwake ni faida kubwa kwa Arsenal ambayo imemnasa.
“Kwa ukweli nimehuzunika sana kumwona Welbeck akiondoka. Hisia zangu ni kwamba kama angefanikiwa kubaki katika dirisha hili angeweza kuwa sehemu ya Manchester United kwa miaka michache ijayo,” alisema Scholes.
“Inaonyesha ni kwa kiasi gani Danny anavyoonwa kwa sasa jinsi klabu kubwa kama Arsenal ilivyoamua kumsaini. Atakuwa mchezaji mzuri kwa Arsene Wenger. Danny hawezi kufunga mabao 20 au 25 kwa msimu, lakini anaweza kuipatia Arsenal mabao 10 hadi 15.”
Pamoja na kuondoka kwa Welbeck, Scholes bado ana hamu ya kuona jinsi safu ya ushambuliaji ya United yenye Wayne Rooney, Robin van Persie na Falcao itakavyozinyanyasa safu nyingi za ulinzi katika Ligi Kuu England.
“Nilimtazama Radamel Falcao akiwa Porto, Atletico Madrid na Monaco niliona jinsi alivyokuwa na mienendo ya hatari na rekodi za ufungaji. Kwa United, uhamisho wake wa mkopo unaleta ushindani mkubwa,” aliongeza Scholes.
“Hata hivyo, sioni namna ambavyo Louis van Gaal anaweza kuwapanga wote watatu, Rooney, Robin van Persie na Falcao kwa pamoja. Inabidi achague wawili kutoka kwa watatu na ni wawili gani hao? Ni vigumu kusema.
“Sidhani kama wanaweza kutwaa ubingwa wa ligi lakini kuingia Ligi ya Mabingwa Ulaya inawezekana. Ni juu ya Van Gaal kuitengeneza timu.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment