Sunday, 27 July 2014

Taarifa ya kesi za kusambaza picha za utupu, kuuza binadamu, vitisho, zilizofunguliwa dhidi ya Eto’o




Huu unaweza sio mwaka mzuri kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto’o, baada ya timu yake ya taifa kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la dunia, na akiwa hana timu ya klabu ya kuichezea baada ya kumaliza mkataba wake na Chelsea, sasa amefunguliwa kesi nzito mahakamani.

Kesi hizo za udhalilishaji kwa kusambaza picha za utupu, vitisho, ununuzi/uuzaji wa binadamu, udanganyifu, na vitisho zimefunguliwa kwenye mahakama moja jijini Yaounde, Cameroon, na aliyekuwa mchumba wa mshambuliaji wa huyo za zamani wa Chelsea, Hélène Nathalie Koah.

Mapema wiki iliyopita Koah alifungua kesi hizo dhidi ya Eto’o ambaye amekana mashtaka hayo.

Hatua hiyo ya imekuja siku chache baada ya kusambaa kwa picha zake za utupu kwenye mtandao Facebook, ambazo mhudumu huyo wa zamani wa ndege amesema zimesambazwa na Eto’o aliyekuwa mpenzi wake.

Eto’o amekanusha kuhusika na mchezo huo mchafu, na katika kujibu mapigo mchezaji huyo anayeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi za uchezaji bora barani Afrika, amefungua kesi ya matumizi mabaya ya fedha($410,755) alizompa Ms Koah kwa ajili ya kufungua taasisi ya kusaidia jamii wakati walipokuwa wapenzi.

Mwanamke huyu alishawahi kuwaingiza kwenye beef mwanamuziki Fally Ipupa na Eto’o kwa kuwachanganya kimapenzi.

No comments:

Post a Comment