Sunday, 27 July 2014

Hussein Machozi afumaniwa akizini na mke wa mwanasiasa maarufu Kenya


Hussein Machozi afumaniwa akizini na mke wa mwanasiasa maarufu Keny

Hit maker wa ‘Kwa Ajili Yako’, Hussein Machozi aliyekuwa ameweka kambi na kukubalika sana nchini Kenya anadaiwa kuwa amefumaniwa na mke wa mwanasiasa wa nchini humo na kupewa masaa 24 kuvuka mpaka wa Kenya.

Kwa mujibu wa gazeti la The Star la Kenya, Hussein Machozi alikuwa anatembea na mwanamke wa mwanasiasa huyo wa Mombasa kwa muda mrefu kwa siri huku wakiwa na mipango mikubwa ikiwa ni pamoja na kununua nyumba.

Lakini mapenzi ni kikohozi, siri hiyo ilimfikia mwanasiasa huyo baada ya kushtukia pale alipoona ujumbe usio wa kawaida kwenye simu ya mkewe kwa njia ya WhatsApp.

Mwanasiasa huyo ambaye anadaiwa kuwa mtu anaesafiri mara kwa mara kufanya biashara na kushughulikia mambo ya siasa aliamua kuweka mtego ambao ulimnasa mwizi wake na kumtia mikononi mwake.

Gazeti hilo linaeleza kuwa liliongea na rafiki wa karibu wa Hussein Machozi wa Mombasa anaefahamika kwa jina maarufu Notystee na alikiri kutokea kwa tukio hilo.



“Nilishtuka pale nilipopokea simu kutoka kwa Hussein Machozi akiniambia kuwa alikuwa katika tatizo. Aliniambia mapema kuwa anaenda kukutana na mwanamke ambaye alikuwa mpenzi wake lakini sikujua kitu ambacho kingetokea.”

Hata hivyo, Hussein Machozi anaonekana bado yuko nchini Kenya kwa mujibu wa chanzo chetu.

No comments:

Post a Comment