Friday, 6 June 2014

MBEYA CITY HIYOOOOOOOO YASAINI MKATABA WA UDHAMINI KWA MILIONI 360 NA BINSLUM.




Wachezaji wa Mbeya City wakiwa mazoezini.

Timu ya mpira wa miguu ya jijini Mbeya maalufu kama Mbeya City FC (WABISHI) wameingia mkataba wa miaka 2 wa udhamini wa timu hiyo ya ligi kuu Tanzania na kampuni ya Binslum Tyre Company Ltd.

Binslum Tyre Company Ltd inayo mirikiwa na Mohamed Bimnslum imeingia mkataba huo kwa gharama za Tsh. 360 Milioni kwa miaka miwili kuanzia msimu huu.

Mohamed Bimnslum ameamua kumwaga pesa zake katika klabu hiyo ya jiji la Mbeya ambayo ilipanda ligi kuu mwaka jana na kuleta upinzani mkubwa baada ya kusumbuana na uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga ambayo alikuwa anaidhamini toka mwanzo.

“Kwa kutambua hilo tumeamua kuidhamini timu ya mpira wa miguu ya Mbeya City ya jijini hapa kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni mia tatu na sitini (360,000,000)” Amesema Mkurugenzi wa Binslum Tyre Company Ltd, Ndugu Mohamed Binslum alipokuwa kwenye sherehe ya makabidhiano na wamiriki wa timu hiyo jijini Mbeya.

“Udhamini huu ambao ni wa kwanza kwa Kampuni yetu kudhamini timu za nje ya Dar Es Salaam unalenga kuiimarisha timu ya Mbeya City ili kufanya vizuri zaidi katika ligi kuu kwa misimu ijayo, pia kuendeleza mpira wa miguu hapa jijini na Tanzania Kwa ujumla” Ameongezea Binslum.

Kwa mkataba huo sasa Mbeya City msimu huu itakuwa inatangaza betri za RB katika jezi kwa mbele kama ilivyo sheria kuwa mdhamini mkubwa wa timu logo au bidhaa yake inakuwa mbele ya jezi.

Mbeya City sasa itakuwa na mafanikio makubwa baada ya kupata udhamini huo huku ikiwa chini ya uangalizi wa manispaa ya jiji la Mbeya.

“Pia ni njia mojawapo ya kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu makampuni kujikita katika kudhamini michezo mbalimbali hapa nchini” Amemalizia Binslum.

No comments:

Post a Comment