Serikali ya Uchina imetoa hizi picha zilizonaswa na mtambo wake wa satelite zikionyesha mabaki ya kitu kipana kikielea katika bahari ya Kusini mwa Uchina. Picha zimepigwa jumapili saa 24 baada ya ndege ya abiria ya Malaysia kutoweka ikiwa na abiria 239. Hakuna uhakika vifaa hivyo ni ndege hiyo.
Fahamu ndege ina raia wa Malaysia 154, ambao walikuwa abiria kwenye ndege hiyo na pia serikali ya Uchina imetuma mitambo 10 ya satellite kusaidia katika harakati za kutafuta ndege hiyo.
Picha za vifaa hivyo 3, ambavyo moja ina upana wa takriban mita 24 kwa 22, zilichukuliwa siku ya Jumapili, siku moja tu baada ya ndege hiyo kupotea, lakini zilichapishwa siku ya Jumatano
Ubawa wa ndege hiyo iliyopotea ina upana wa mita sitini na moja.
Picha za satellite zimeweka vifaa hivyo takriban maili 100 kutoka kwenye njia iliyotarajiwa kutumiwa na ndege hiyo na sio mbali kutoka kwa kisima kimoja cha mafuta, ambako mfanyakazi mmoja aliripoti kuona kitu kilichokuwa kikichomeka angani siku ya Jumamosi asubuhi. Makundi ya uokoaji yanaendelea kutafuta mabaki ya ndege hiyo.
Source BBC
No comments:
Post a Comment