
Wabumge wameanza kuingia Ukumbini. Ndani ya Ukumbi wa Bunge, idadi ya Wabunge ni ndogo dakika 10 kabla ya Kikao Kuanza.
- Wagombea waliotimiza vigezo vya kugombea ni wawili tu na wengineo hawapo tena katika kinyang'anyiro hicho. Waliokidhi vigezo kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba; Samwel J. Sitta na Hashim Rungwe!
- Kila mgombea anapewa nafasi ya Dakika tatu kujieleza kisha yatafuata maswali. Anaanza kujieleza Hashim Rungwe.
* Rungwe kamaliza kujieleza; zaidi amedai yeye ni Mtanzania wa kwanza kuwa na Yard ya Magari mwishoni mwa miaka ya 80 na yeye ni Wakili wa Kujitegemea wa Mahakama Kuu ya Tanzania
* Sitta kajieleza wasifu wake kwa ufupi na kuwahakikishia wajumbe kuwa hatapendelea upande wowote. Anataka kuwahakikishia watanzania kuwa wataona sababu ya wajumbe kupewa hata kiinua mgongo watakapomaliza zoezi hili. Kasema yeye kupewa kiti ni sawa na kumrudisha chura kwenye maji, ni wazi ataogelea tu!
source jamii forum
No comments:
Post a Comment