Monday, 3 February 2014

Unadhani Manchester United itafuzu kucheza Champions League msimu ujao, Smalling atoa ya moyoni.





Beki wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Chris Smalling ameelezea hisia zake juu ya kiwango cha timu yao hivi sasa, akitoa ishara kwamba kikosi cha David Moyes kinahitaji kushinda kila mechi katika zote zilizobakia ikiwa wanahitaji kuweza kupata nafasi ya kushiriki michuano ya mabingwa wa ulaya msimu ujao.



United walipokea kipigo cha 2-1 jumamosi kutoka kwa Stoke, kipigo chao cha 8 msimu, na sasa wanashika nafasi ya 7 pointi nne nyuma ya timu inayoshika nafasi ya nne Liverpool.

Hata hivyo, Smalling amekiri kwamba United wanaweza kushindwa kufuzu kucheza michuano ya mabingwa wa ulaya; ikiwa watashindwa kufanya hivyo, itakuwa ni mara ya kwanza katika miaka 19 kwa klabu hiyo kutoshiriki michuano hiyo mikubwa kabisa kwa ngazi ya vilabu barani ulaya.

“Inabidi tushinde kila mchezo uliobakia,” Smalling aliiambia theMirror. “Hatupaswi kupoteza mechi tena namna hii, hatupo katika nafasi nzuri, inabidi tuwe na wasiwasi na kujitahidi kucheza vizuri na kushinda kila mechi.

“Kuna vitu vingi vitaendelea, lakini muda haupo upande wetu na inabidi tuhakikishe tunarekebisha makosa katika mchezo ujao. Vinginevyo hali itakuwa ngumu sana kuweza angalau kufuzu kushiriki champions league.”

No comments:

Post a Comment