He is a Ordinary Diploma Of Computer Science also holder of BSc(Cs)Bachelor of Science in Computer Science from ST. .JOSEPH UNIVERSITY to RUCU. The C.E.O and founder of I.T MAN SOLUTION Tz1 with enough knowledge in Computer mainteance and softwares, android tricks, web designing and graphics design, part-time blogger and softwares distributor with enough knowledge on entrepreneurship. Reach him 24/7 through WhatsApp 0716 68 43 67 and 0762324735 itmansolution2016@gmail.com.
Monday, 17 February 2014
SOMa STORI YA KUSIKITISHA INAYOMUHUSU MSANII AT
‘Everyone has a story to tell’, huu ni msemo uliotumiwa na waandishi wengi wa habari wakongwe na maarufu duniani waliojikita katika habari za masimulizi ya binadamu, msemo au motto uliomsaidia mpiga picha Lisa Rivers mwaka jana kutengeneza Makala nzuri ya picha ya inayotokana na story ya maisha yake kikazi.
Msemo au motto huu umetumiwa na Tovuti ya Times Fm na kufanikisha kupata simulizi kubwa na la kusikitisha kutoka kwa muimbaji wa ‘Nipigie’, mzaliwa wa Zanzibar, AT.
Sio tu simulizi la kusikitisha, pia tovuti hii imeweza kupata simulizi la kushangaza na linaloihusu ndoa ya bwana Ally aka AT.
Tukianza na simulizi la kusikitisha ambalo tunaweza kulitaja kama ‘simulizi la kusikitisha zaidi la uhalisia lililowahi kusimuliwa kwenye media na msanii mkubwa wa Tanzania. Hata hivyo msanii huyo aliiambia tovuti ya Times Fm kuwa hakuwahi hata siku moja kuyaweka masimulizi haya kwenye media wala kumsimulia mtu asiye wa familia yao.
Hii ni kwa ajili yako, tunaanza na simulizi la kwanza:
Mimi nina kitu ambacho nadhani watanzania wengi hawakijui na ni kwa sababu sijawahi kukizungumza kokote ila tu ni kwa heshima yenu na heshima ya watanzania. Mimi nimeanza kutembea nikiwa na umri wa miaka mitano.
Tangu nilipozaliwa nilikuwa tu nipo, natambaa kama kawaida lakini baada ya miaka mitano ndio nikaanza kutembea kwa sababu nilikuja nikaumwa mpaka hakuna aliyeweza kufikiria kama ningepona katika familia na mwili wangu ulikuwa una usaha mwili mzima. Mfano, ukichukua wembe ukichinja kwenye mwili haitoki damu inatoka usaha, kwa hiyo kitu ambacho kilikuwa kinapelekea watu wanashindwa kukaa kwa sababu ya harufu, ulikuwa unatoa harufu sana.
Mama yangu mwenyewe siku moja aliwasikia watu wanazungumza kuwa huyu mtoto hawezi kupona, kama sio kesho basi kesho kutwa tunaenda kuzika. Kitu ambacho wamekuja kushangaa baada ya kuja kuniona mimi mzima na nakwenda. Lakini nimeanza kutembea nina miaka 5, watoto walikuwa wananishangaa jitu zima najifundisha kwenda. Wenyewe watoto wadogo wanaenda nawekwa nichezeze nao lakini siwezi nalia, inabidi watoke watu waje kunichukua.
Yaani hakuna mtu hata mmoja anaamini kwamba yule mtoto ambaye alikuwa anaumwa tukawa tunafikiria marehemu, leo hii atajulikana Tanzania nzima na atakuwa mtu maarufu na anafanya shughuli zake anaruka na kucheza.
Na ilikuwa inafikiria kipindi, kama mvua inataka kunyesha wiki moja kabla watu wanatizama majira kupitia mimi, miguu yangu kwanza lazima ivimbe, na ukibonyeza hivi kama umebonyeza mkate halafu inakuja juu taratibu. Kwa hiyo watu walikuwa wakiniona niko hivyo wanajua kuwa mvua inataka kunyesha. Kwa hiyo nilikuwa kama mtoto wa ajabu ajabu.
Lakini alikuja doctor mmoja mpaka leo yu hai anaitwa ‘Makwetu’ ndio aliweza kunitibia, tungekuwa tuna imani kama hizi za sasa hivi tunazungumzia za kishirikina basi mimi ningeweza kufa. Nilichanwa kwenye mguu kwenye miguu mpaka leo niko na kovu, nikatiwa vyuma, ikapanuliwa mifupa ya miguu, ulitoka usaa naambiwa unaweza kufika hata ndoo, yaani mwili mzima mpaka mikononi nikawa natiwa mautambi….mpaka watu wanaulizana kulikoni, karogwa au vipi. Lakini mwenyezi Mungu ndio ana mipango yake, hakuna mtu anaweza kujua.
Kwa hiyo iliwapa ugumu sana wazazi wangu, lakini baba yangu kipindi hicho alikuwa nje (Ugiriki), na alikuwa amekata tamaa kabisa, anajua huyu mtoto ni marehemu.
Hata hivyo, mwimbaji huyo aliyenusurika kifo kwa ugonjwa huo mbaya, analo simulizi lingine la kweli kuhusu maisha yake, simulizi la kushangaza lakini linaweza kuwa lilimfuta majonzi yote baada ya kuambiwa kile asichokifahamu kuhusu uhusiano wake yeye na mkewe.
AT alifunguka kuhusu maajabu ya ndoa yake:
Baba yangu wakati nazaliwa alikuwa na rafiki yake anaitwa Suleiman, akamwambia mimi nimepata mtoto wa kiume. Akamwambia ‘daah wewe umepata mtoto wa kiume…daah mimi nikipata mtoto wa kike ntakuja kumuozesha mwanao’.
Huwezi kuamini, wakati nimeenda kuposa mke wangu ambaye mimi nimemuoa…ni kwa mara ya kwanza nasema, ni yule mtoto ambaye baba yangu na baba yake walizungumza wakati wako Ulaya (Ugiriki) kwamba wataozeshana na hawakujua sisi tumeonanaje!
Hadi baba yangu akashangaa, wakaambizana kwa kweli Mwenyezi Mungu yupo,‘bwana Suleiman, tulizungumza kwamba utanipa mtoto wako wa kike mwanangu wa kiume amuoe, mtoto mwenyewe ndio huyu aliyekuwa akiumwa ndio huyu Ally…’
Kwa hiyo ni kitu ambacho hamna mtu ambaye anajua, najua mimi na mke wangu…kwa hiyo watu wajue hivyo, mimi na mke wangu ni watu ambao wazazi watu ni marafiki na walizungumza wakati wako Ugiriki...na ndio sababu nampenda mke wangu.
AT amesema kuwa hivi sasa yeye na mkewe wameshajaliwa kuwa na mtoto mmoja, lakini maajabu hayaishi, yapo pia katika tarehe ya kuzaliwa ya familia yao.
Yaani yeye, baba yake na dada yake wamezaliwa tarehe moja..wanasherehekea siku moja ya kuzaliwa (Tarehe 19 mwezi wa nane).
AT anaamini kutokana na simulizi la maisha yake, Mungu alikuwa amemuandaa kuwa mshindi tangu mapema. Huyu ndiye AT, mshindi wa tuzo ya Kili aliyejizolea mashabiki wengi kwa wimbo wake ‘Nipigie’ akiwa na Stara Thomas.
SIKILIZA HAPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment