Tuesday, 4 February 2014

SOMA ANACHOTAKA KUKIFANYA MSANII DAIMOND NI NOUMAAAAAAAAAA


 millardayo.com inazotaarifa za chinichini kwamba single ya ‘number one rmx’ ya Diamond Platnumz ft Davido wa Nigeria ipo kwenye mstari wa kuingiza mkwanja kupitia mauzo ya mlio kwenye simu, yani Wanigeria wenyewe wanaitaka.
Pamoja na Diamond kutajwa kuwa msanii wa bongofleva anaeingiza pesa nyingi kwa miaka miwili mfululizo kila mwezi kutokana na show zake anazotoza mamilioni ya Kitanzania, mpango mwingine alionao ni kufanya biashara za mavazi kupitia jina lake.

Unaambiwa mzigo wa kwanza wa mavazi ya jina lake tayari ulitoka ila aliukataa kutokana na kuwa na kiwango cha chini hivyo ikabidi atoe oda nyingine hukohuko China alikoagiza mzigo wa kwanza.

Pamoja na hizo harakati za kunenepesha bank, inaonekana Diamond Platnumz anawaza kuishi kistaa au kifahari zaidi kama wanavyofanya mastaa wengine wa dunia manake kapost hiyo picha hapo juu kwenye mitandao yake ya kijamii na kisha akaandika haya maneno hapa chini...

No comments:

Post a Comment