Wenger hapati jibu juu ya uamuzi wa Mourinho kukubali kumpeleka Mata kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England.
LONDON, ENGLAND
KOCHA, Arsene Wenger wa Arsenal hajapata jibu na
bado anajiuliza kama akili ya Jose Mourinho inafanya kazi sawasawa
kutokana na uamuzi wake wa kuwauzia Manchester United mchezaji Juan
Mata.
Wenger hapati jibu juu ya uamuzi wa Mourinho kukubali kumpeleka Mata kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England.
Staa huyo Mhispaniola amekamilisha vipimo vya afya
kwa ajili ya kujiunga Man United baada ya kukosa nafasi ya kucheza
kwenye klabu ya Chelsea licha ya kuwahi kuwa mchezaji bora wa kikosi
hicho kwa misimu miwili mfululizo kabla ya kurejea kwa Mourinho klabuni
hapo.
Man United kwa sasa inajaribu kuboresha kikosi
chao baada ya kuanza msimu vibaya wakiwa nafasi ya saba kwenye msimamo,
pointi sita pungufu kuwamo kwenye nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa
Ulaya msimu ujao.
Wenger alisema: “Nimeshangazwa sana Mata
ameruhusiwa aondoke. Chelsea imewanufaisha moja kwa moja wapinzani. Hivi
Chelsea haitacheza tena na Man United. Wangemuuza Mata basi wiki mbili
zilizopita.” Mfaransa huyo Jumatano iliyopita alikuwa Hispania
kuzitazama Barcelona na Levante zikimenyana kwenye Kombe la Mfalme ikiwa
ni safari yake ya kusaka straika mpya.
No comments:
Post a Comment