He is a Ordinary Diploma Of Computer Science also holder of BSc(Cs)Bachelor of Science in Computer Science from ST. .JOSEPH UNIVERSITY to RUCU. The C.E.O and founder of I.T MAN SOLUTION Tz1 with enough knowledge in Computer mainteance and softwares, android tricks, web designing and graphics design, part-time blogger and softwares distributor with enough knowledge on entrepreneurship. Reach him 24/7 through WhatsApp 0716 68 43 67 and 0762324735 itmansolution2016@gmail.com.
Thursday, 9 January 2014
WASTARA: NATAKA KUOLEWA NA BILIONEA.
IKIWA ni takribani mwaka mmoja tangu alipoondokewa na mumewe, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amesema sasa yupo tayari kuolewa lakini sharti la kwanza la muoaji lazima awe mtu mwenye fedha zake.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Wastara alisema, amekuwa mpweke kwa muda mrefu na sasa ni wakati muafaka wa kumpata mtu wa kuziba pengo la marehemu mume wake
“Inatosha sasa, nadhani muda wa kuwa na mwenzangu umefika. Napenda huyo mwanaume awe mwenye huruma, upendo na kutambua thamani ya mke lakini ni vizuri akiwa mwenye kujituma na awe na fedha nyingi.
“Natamani kuolewa na bilionea. Najua nikiwa na mwanaume wa aina hiyo sitateseka, nitapata kila ninachokitaka. Unajua mimi kama mwanamke nina mambo mengi. Siyo siri natamani itokee siku moja niendeshe Hummer au Prado (aina za magari) kulingana na hadhi yangu.
“Kiukweli nitafurahi sana nikimpata mwanaume wa aina hiyo, maana nitakuwa na uhakika wa kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kunisaidia katika shughuli zangu za sanaa,” alisema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment