Wednesday, 22 January 2014

NEWS: MABOMU YA LINDIMA CHUO CHA MTAKATIFU JOSEPH SONGEA; RAISI WA CHUO AVUNJWA MGUU

EXCLUSSIVE NEWS: MABOMU YA LINDIMA CHUO CHA MTAKATIFU JOSEPH SONGEA; RAISI WA CHUO AVUNJWA MGUU.



 Habari zilizo tufikia majira ya asubuhi polis wamewalipua mabomu wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph tawi la Songea. Tukio hili limetokea makao makuu ya tawi la chuo cha St.Joseph Ruhuwiko. Raisi wa serikali ya wanachuo ndugu Alistide Mujwauzi amevunjwa mguu na polisi baada ya kipigo kikali na wengine wana majeruhi kutokana na virungu vya polisi. Hadi hivi sasa kuna wanafunzi wanashikiliwa na polis. MWAMWAMWA baada ya kuwasiliana na wanafunzi walio tupasha habari hii kwa njia ya e-mail wameandika “Hata vyombo vya habari naisi vinapewa bahasha na hawa Wahindi maana mtangazaji wa TBC Greyson Msigwa mara nyingi anakuja kutupiga picha lakini hatuoni ni wapi zinaonekana sasa sijui anataka haionyeshe familia yake nyumba. Ndugu yangu hapa tunavyochat kuna wana chuo hawajui pa kulala maana kuanzia asubuhi mpaka saa hivi polisi wanapita Nyumba hadi nyumba eneo la Ruhiwiko chuo kilipo kuulizia kama kuna mwana chuo anaishi hapo. Sasa ebu vuta picha kwa watoto wa kike” Anaendelea… “Cha ajabu matatizo yote haya tumeyaongea sana na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya songea Ndg. Mkirikiti lakin wakiwa nasi tunaongea lakini wakienda chuoni kukutana na uongozi wa chuo wakija wanakuwa wapole na hakuna la maana wanaloongea tunaishi kuna bahasha inatembea maana hata TCU wanishia kuifungia Kampala university wakati chuo chetu hata hawa Ma lecturers ni wabovu tena iweje karibia asilimia 95 ni wahindi huu ni uwekezaji gani. Ndugu yangu naomba mtusaidie maana mpaka sasa wenzetu wako polisi na kuanzia RC na DC hakuna mtu namba yake ya simu inayopatikana nyinyi tunatambua ni watetezi wa wanyonge tusaidieni sisi watoto wa masikini tunaonyanyaswa kwenye ardhi yetu na hawa wawekezaji uchwara wa Kihindi. Anaendelea kutoa malalamiko… “Pia uongozi wa chuo unatabia ya kubadilisha course kwa mfano mwaka 1 na 2 wamebadilishiwa course yao ambayo walichaguliwa na TCU licha ya hivyo mpaka leo mwaka wa pili hawajapewa score sheet (matokeo) ya semister mbili yaani tangu wameanza chuo. Pia chuo na break system kwa mtu ambaye anashinda Kuiondoa sup yake yaan anakaa nyumbani mwaka mzima mpaka afanye vziur hy sup yk lkn cha ajabu hela yk ya mkopo inaletwa kumbe hawa Wahindi kabla ujafanya UE wao wanapeleka matokeo bodi umefaulu wakati huku wamekupiga break uwezi amini hapa hata uwe unaumwa maututi hakuna special paper yaani mtu anajifungua jana leo anafanya mtihani” TAKE AWAY: -Raisi wa serikali ya wanachuo ndugu Alistide Mujwauzi amevunjwa mguu na polisi - Wengine wana majeruhi kutokana na virungu vya polisi. -Hadi hivi sasa kuna wanafunzi wanashikiliwa na polisi

No comments:

Post a Comment