Wednesday, 29 January 2014

Mchungaji Gwajima atabiri Sitta na Mwakyembe kuhamia CHADEMA na CHADEMA Kushinda 2015



Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Kawe, Mch.Josephat Gwajima amesema Tanzania mpya yenye matumaini inakuja.

Akihubiri Kanisani hapo leo alisema ingawa yeye ni mwana CCM na vyombo vyote vilivyotumika kwenye mkutano wa ccm Jangwani jana vilitoka Kanisani kwake, alisema chama cha siasa cha ccm kipo katika wakati mgumu na kimepoteza kabisa mwelekeo na uwezo wa kuongoza dola.

Amewaonya wanasiasa wanaojiona ni wasafi na bado wanang'ang'ania ccm, wajue mwisho wao kisiasa upo ukingoni, aliwaonya Mwakyembe, Sita na wanasiasa wangine kuwa hali ya ccm ilivyo sasa ni sawasawa na samaki aliye ndani ya bwawa na maji ambalo linakaribia kukauka.

"Tanzania mpya inakuja" ulikuwa ndio ujumbe wake wa leo.

Tanzania yenye uwezo wa kukomesha rushwa inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kujali afya za wananchi wake inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kukomesha wizi wa mali za uma inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kuwapatia vijana wake elimu bora inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kuwalisha wananchi wake inakuja.

Amewatakia wananchi wote afya njema, wapate kuipokea Tanzania mpya.

Tanzania mpya inakuja - AMINA.

No comments:

Post a Comment