Friday, 10 January 2014

MASOGANGE ANASWA NA MPENZI WA JACKIE CLIFF





VIDEO Queen, Agnes Jerald ‘Masogange’ hivi karibuni alibambwa maeneo ya Sinza Kamanyola jijini Dar akijiachia na anayetajwa kuwa ni mpenzi wa Jack Patrick, Juma Khalid ‘Jux’.


Wawili hao walibambwa kwenye duka moja lililopo maeneo hayo baada ya Jux kutua kutoka China huku Agnes akionekana kama anayemfariji kwa tukio la Jack kunaswa na madawa ya kulevya.

Akiuzungumzia ukaribu wake na Jux, Masogange alisema: “Wala hakuna lolote kati yangu na yeye. Mimi na wale akina Jux pamoja na dada yake ni watu wangu wa karibu sana tunaojuana muda mrefu hivyo tulikuwa tunabadilishana mawazo tu.”

Jux na Jack wamekuwa wakionekana katika mitaa ya China wakila bata huku kukiwa na madai kuwa ni wapenzi na kuonekana kwa Jux na Masogange wakijiachia kumeibua maswali mengi

No comments:

Post a Comment