Thursday, 9 January 2014

LOWASA AWAJIBU NAPE NA MANGULA SOMA HAPA ALICHOKISEMA

Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Mh. Edward Lowassa, ametembelea miradi ya maji katika kata ya Selela iliyopo Jimbo lake la Mondul na kuongea na wapiga kura wake na kuwapiga vijembe viongozi wa chama chake waliomwambia watamchukulia hatua kali kwa sababu ya kutangaza nia ya kugombea kiti cha urais mwanzoni mwa mwezi hata kwa chama JIWE atakuwa rais 2015.








Mh. Lowasa aliwakumbusha akina Nape na Mangula kwamba yeye Uwezo anao, nia anayo, wananchi wananipenda wakanitangazia siyo mimi nimetangaza na kuhusu harambee nimechangia kama wenzangu wanavyochangia, au nikiitwa kwenye harambee nisishiriki mpaka uchaguzi wa rais 2015 upite? Hiyo ni adhabu. Tuwe wangalifu na kuchambua maneno, Tusiwe wepesi kulaumu na kuhukumu na pia kuwa kiongozi siyo kutisha na kuogopesha wanachama, wote tuna haki sawa katika chama chetu.

Ni hivi majuzi viongozi wa juu wa CCM walimuonya Lowasa na wananchama wengine wa chama hicho kuacha kujitangazia kuwania urais kupitia CCM kwa vile muda wake rasimi bado na pia kutoa michango ya harambee mbali mbali, na kwa kufanya hivyo ni kuvunja kanuni, sheria za mwongozo wa chama na adhabu yake ni ku-jiqualify automatically wenyewe kwenye kuwania urais.

No comments:

Post a Comment