Thursday, 23 January 2014

JUANA MATA ATUA MANCHESTER UNITED KWA DAU NONO



Klabu ya Manchester United imekamilisha usajili wa Juan Mata kutoka Chelsea kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya kiasi cha pauni milioni 40.

Kiungo huyo alikosa mazoezi ya Chelsea jana Jumatano ikiwa ni hatua ya kwanza ya kukamilisha uhamisho huo huku akisafiri kuelekea mjini Manchester kufanya mazungumzo.

Uhamisho huo wa Mata umekuwa wa kwanza mkubwa zaidi kufanyika katika kipindi hiki cha Januari.

Mhispania huyo aliwaambia marafiki zake kuwa anaondoka Stamford Bridge,ingawa meneja,David Moyes alikataa kuzungumzia uhamisho huo mara baada ya kushuhudia kikosi chake kikifungwa kwa penati na Sunderland katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Capital One kwenye dimba la Old Trafford.

Nyota huyo anataraji kufanya vipimo vya afya kabla ya wikiendi hii katika klabu hiyo ambayo msimu huu inatetea Ubingwa wake wa ligi kuu ya Uingereza

Man United inahitaji kuimarisha kikosi chake kutokana na kuwa na msimu mbaya na kusajiliwa kwa Mata kwa dau lililovunja rekodi ya klabu hiyo ni nia ya kutaka kukirudisha timu kwenye ushindani na kiwango kizuri.

Chelsea wameridhika kufanya uhamisho huo kwani,Jose Mourinho ana viungo washambuliaji wengi katika kikosi chake hivyo imekuwa njia sahihi ya kumridhisha kiungo huyo ambaye alisajiliwa akitokea Valencia mwaka 2011 kwa kiasi cha pauni milioni 23.5.

No comments:

Post a Comment