Friday, 10 January 2014

BABY MADAHA 'AWACHANA' WASANII WANAOJIVUNIA ZIARA ZA NJE YA NCHI.



Msanii wa filamu ambaye pia ni mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Baby Madaha ambaye yupo chini ya kampuni inayojulikana kwa jina la Candy n Candy amefafanua kuwa msanii hatakiwi kutumia kigezo cha kufanya ziara nje ya nchi kama ukuaji wa muziki wake.
Akizungumza na Pro -24 ,muda huu Madaha aliweka wazi kuwa wasanii hawatakiwi kuchukua kigezo cha kufanya ziara ndio kukua kimuziki na badala yake wanatakiwa wajipime na uwezo wao na jinsi muziki huo unavyosikika nje ya nchi.
Aliweka wazi kuwa kufanya ziara si sababu ya kumfanya msanii huyo kuonekana ameingia katika anga za kimataifa na badala yake wanatakiwa wajikite zaidi katika kuuza muziki huo kuhakikisha wanapata nafasi ya muziki wao kusikika katika nchi nyingine.

No comments:

Post a Comment