He is a Ordinary Diploma Of Computer Science also holder of BSc(Cs)Bachelor of Science in Computer Science from ST. .JOSEPH UNIVERSITY to RUCU. The C.E.O and founder of I.T MAN SOLUTION Tz1 with enough knowledge in Computer mainteance and softwares, android tricks, web designing and graphics design, part-time blogger and softwares distributor with enough knowledge on entrepreneurship. Reach him 24/7 through WhatsApp 0716 68 43 67 and 0762324735 itmansolution2016@gmail.com.
Monday, 30 December 2013
JEURI YA FEDHA BEYONCE NA JAYZ WATUMIA MILION 158 KUNUNUA VINJWAJI
Jeuri ya pesa inaonekana kwa couple ya Jay Z na Beyonce ambayo imetajwa kuwa imeingiza mkwanja mrefu zaidi kuliko couple yoyote ya wanamuziki.
Ijumaa (December 27), wawili hao walitumia kiasi cha $100,000 (zaidi ya shilingi milioni 158 za Tanzania) kwa ajili ya kununua vinywaji katika club ya usiku ya ‘Rein’ huko Atlanta.
Kwa mujibu wa TMZ, wawili hao walitumia kiasi hicho cha pesa kuwanunulia vinywaji watu wote waliokuwa VIP, ambapo wasanii wenzao kama Bow Wow, Jermaine Dupri, Dream na Trey Songz walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa VIP kuwapa kampani.
Jay-Z na Beyonce walikuwa wakipongezana kufuatia kufanikiwa sana kwa album ya Beyonce aliyoipa jina lake, lakini pia kutajwa kwa Jay-Z kuwania tuzo ya Grammy katika vingele 9.
Katika habari nyingine, Queen Bey amefunguka katika videoya Part 3 Run ‘N Gun’, na kusema kuwa yeye na producer wa Drunk In Love walikunywa pombe ‘Dusse’ wakati wanarekodi ngoma hiyo, na kwamba ni kama alifanya freestyle kwenye verse.
“Ni kama nilifreestyle ile verse, na Jay akaingia na akaanza kuflow verse yake.” Amesema Beyonce. “Ni kama tulikuwa na party. Ilikuwa poa sana, kwa sababu hakukua na ubinafsi, hatukuwa tunajaribu kufanya hit , tulikuwa tunajaribu kufurahi na nadhani unaweza kusikia kwenye wimbo.” Ameongeza.
Drunk in Love ni wimbo unaopatikana kwenye album yake ‘Beyonce’ ambao amefanya na mumewe Jay Z, video ya wimbo huo ina shots kadhaa zenye mvuto wa mahaba zilizochukuliwa ufukweni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment