Tuesday, 24 December 2013

Hivi Ndivyo Miss Tanzania Happiness Watimanywa Atatumia Siku Yake Ya Krismasi




Hivi Ndivyo Miss Tanzania Happiness Watimanywa Atatumia Siku Yake Ya Krismasi


Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa, Krismasi hii atajumuika na watoto yatima wa kituo cha Mgolole Orphanage kilichopo Bigwa nje kidogo ya Mji wa Morogoro.

Mrembo huo ataungana na warembo wengine watatu, akiwemo Miss Tanzania mshindi wa pili Latifa Mohamed, Miss Tanzania mshindi wa tano Elizabeth Perrty, na Sabra Islam Miss Morogoro 2013 ambaye ndie atakae kuwa mwenyeji wao wakati wote wakiwa mkoani hapo.


Afisa Uhusiano Lino International Agency Hidan Ricco amesema ni kawaida kwa Mrembo wa Taifa, Miss Tanzania kila mwishoni mwa mwaka kula Krismasi na Watoto Yatima, wasiojiweza pamoja na wale waishio katika mazingira magumu.


Baada ya shughuli hiyo Miss Tanzania Happiness Watimanywa atajumuika pia na watoto wa aina hiyo jijini Dar es Salaam siku ya Mwaka mpya tarehe 1 January 2014 katika vituo vingine atakavyopangiwa na Kamati ya Miss Tanzania.





No comments:

Post a Comment