Sunday, 29 December 2013

FEZZA ATIMKA BOTSWANA WAJUA ALIKOTIMKIA

11

Ni mrembo wa Kitanzania ambae aliiwakilisha nchi kwenye shindano la Big Brother Africa 2013 ambapo baada ya kutoka alizimiliki headlines nyingi

kutokana na uhusiano wake wa kimapenzi na mshiriki mwingine wa BBA ambae walikutana kwenye jumba hilo, O’neal kutoka Botswana.

Kwa miezi hii yote ilikua inajulikana Feza yupo Botswana kwa O’neal ambae headlines zilitangaza sana kwamba mapenzi ya wawili hawa yanaweza kuwafikisha mpaka kwenye ndoa.
Sasa basi, mchapo wa leo ni kuhusu info mpya Exclusive on millardayo.com kwamba Feza ameondoka Botswana na kuhamia South Africa ili kujijenga zaidi kimuziki na pia kujitangaza na kuutangaza muziki wenyewe wa bongofleva anaoufanya.
Swali la kwanza nililomuuliza baada ya kusema kahamia SA lilikua >>> Umehamia South Africa na boyfriend wako? akajibu ‘No, niko mwenyewe lakini na yeye kahamia sio mbali sana na hapa, ni majirani’
Swali jingine: Bado mko pamoja kama Wapenzi? akajibu >>> ‘yeah lakini focus ni kazi kwa sana, mbali na muziki nitakua namalizia degree yangu ya Maendeleo ya Jamii huku na pia kuendeleza muziki wangu, nimeshakutana na producers kadhaa kujadili mipango inayofata lakini single yangu inayofata definitely itakua imefanyika Tanzania, bado nataka kufanya bongofleva na kuipaisha huku’
millardayo.com : Umehamishia makazi yako huko moja kwa moja? akajibu >>> ‘Hapana, nitakua part time huku na time nyingine Tanzania’
millardayo.com : Na Boyfriend wako kahamia moja kwa moja South Africa? akajibu >>> ‘Na yeye ana mazungumzo na Radio Stations za huku so atahamia moja kwa moja, sijui zaidi ya hapo’

‘Mimi na mashabiki zangu at Gold Reef City-Theme Park, rocking my new hair….. lol’

Hii picha ya juu ni wakati Feza alipowasili Botswana kwa kina O’neal.

No comments:

Post a Comment