Tuesday, 17 December 2013

Diamond Platnumz kuanzisha studio yake ya kusaidia wasanii wachanga






Diamond Platnumz amesema anaanzisha studio yake mwenyewe itakayokuwa ikiwasaidia wasanii wachanga.

Mkali huyo wa ‘My Number One’, alitoa taarifa hiyo Ijumaa iliyopita wakati akijibu maswali kutoka kwa mashabiki wake waliokuwa wakimuuliza kwenye ukurasa wa Facebook wa kipindi cha Coke Studio Africa.

Akijibu swali la Crown Prince Eric lililouliza: What are you doing to help society even a little pal? Diamond alisema: I am starting a studio which will help upcoming artists and those who want to venture into music.”

Hii ni habari njema kwa wasanii wengi wachanga nchini.

No comments:

Post a Comment