Sunday, 29 December 2013

BABY MADAHA AMCHANA DAIMOND KUWATUMIA WANAWAKE KUINUA MZIKI WAKEE








WIKI kadhaa zilizopita tulisikia msanii wa filamu na muziki Baby Madaha akifunguka na kusema kuwa
Diamond siyo msanii bali ni malaya na anatumia wasichana maarufu ili apate kiki katika muziki anaoufanya. Baby Madaha alizidi kufunguka na kusema endapo wasanii maarufu wa kike wakipata uelewa na wakamgundua Diamond basi ndiyo mwisho wa msanii huyo kusikika hewani.
Madai hayo ya Baby Madaha yanaweza yakawa na ukweli ndani yake kwa hiki ambacho kinaendelea kwa sasa kati ya msanii Diamond na Wema Sepetu.
Diamond hivi karibuni atatambulisha wimbo wake mpya wa Number 1 remix aliyoufanya nchini Nigeria na msanii Davido wa nchini humo, Kulingana na madai ya Baby Madaha yaonekana Diamond anatafuta Kick kwa kutoka na mwanadada Wema Sepetu na mpaka kutambulisha anataka kuoa.

No comments:

Post a Comment