Monday, 20 January 2014

BREAKING NEWS::__Watu sita wafariki Dunia baada ya kuangukiwa na machimbo ya Kokoto (Moram)





Watu sita wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na machimbo ya moram hapa wilayani Karatu.

Machimbo hayo yako karibu na shule ya Sekondari Mlimani. Hali ni tete ni majonzi kila kona.

Habari zaidi zinasema kuwa huenda kuna watu zaidi ndani ya machimbo hayo na mkurugenzi wa Halmashauri ameagiza grader kwaajili ya kuendelea kufukua zaidi.

Hapa wilayani Karatu hakuna kifaa chochote cha uokozi na wala gari la zima moto hakuna. Watu tunaishi kama tuko shimoni.

R.I.P. Vijana 6 wa kitanzania waliofariki katika kutafuta riziki.


No comments:

Post a Comment